The House of Favourite Newspapers

Parimatch Gumzo Kila Kona, Diamond Anogesha!

Kampuni ya michezo ya kubashiri PariMatch Tanzania imekuwa ya kwanza ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuweza kubadilisha mfumo wa michezo ya kubashiri maarufu kama betting kutoka kwenye mtazamo wa aina ya ajira hadi kuwa burudani, kitu ambacho kampuni nyingi zimeshindwa kukabiliana nalo kwa namna moja ama nyingine.

 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi muendeshaji wa kampuni hiyo, Tumaini Maligana alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu na kusema kwamba kwa miaka mingi sekta ya kubashiri imekuwa ikichukuliwa kama michezo ya kihuni au ya watu walio na kipato cha chini bila ya kufahamu kuwa michezo ya kubashiri ni michezo kama ilivyokuwa mingine katika jamii zetu.

Aidha, Maligana amesema kampuni ya Parimatch imejipanga vizuri katika kubadilisha mtazamo wa michezo ya kubashiri Tanzania na ndio maana wameamua kuanzisha kampeni yao rasmi ya BURUDANI ISIYOUMIZA kwa kushirikiana na Balozi wao ambaye ni gwiji wa burudani ndani na nje ya Tanzania, Diamond Platnumz.

 

“Tumechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Diamond kama balozi wetu kwa dhana hii ya Burudani, yeye ni mtu ambaye amepambana na ameweza, Ila kikubwa ni kwamba huwezi ongelea burudani Tanzania bila kumtaja Diamond. Tunaamini kwa nafasi yake ya Ubalozi atasaidia kutoa uelewa kwa wachezaji maana hasa ya kubeti ili wote tuweze kufurahi na kucheza kistarabu”, alisema Maligana.

Pamoja na hayo, Maligana alibanisha baadhi ya mambo kwa kusema kuwa “kutokana na msaada tunaopata kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania ambao kiukweli wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kusimamia na kuhimiza kubeti kistaarabu kupitia kampeni yao ya Makinika kijana, tunawaunga mkono katika jambo hili kwa manufaa ya wateja wetu pamoja wadau wengine mbalimbali”.

 

Vilevile, Mkurugenzi huyo amewataka wadau wa kubashiri wasicheze mbali na Parimatch ili waweze kuwa wakwanza kupata ofa na promosheni mbalimbali ambazo zipo njiani kuachiwa kutoka sasa.

Mbali na hayo, Parimatch Tanzania inaunga mkono juhudi zinazoendeshwa na serikali ya Tanzania katika suala zima la kutunza mazingira na kuamua kutupilia mbali mfumo wa kizamani wa kutumia makaratasi katika mikeka na badala yake wao hutumia njia ya kidigital katika kufanya ubashiri kwa kadi ama mtandaoni kwa dau dogo tu la shilingi 300 huku wakikuruhusu kuweka mkeka wa hata mechi moja tu.

Kwa hakika Parimatch Tanzania ni kampuni yenye upekee kuanzia hata mtazamo wa maduka, wamekuwa tofauti kabisa na tulivyozoea kuona maduka ya wakamaria yakiwa hovyo hovyo, kutokana na uchafu wa makaratasi yaliyozagaa pamoja mambo mengine. Kutokana na hilo Parimatch wameamua kutumia mfumo wa kompyuta ambapo kila mchezaji mmoja huwa na yake wakati wa kuweka ubashiri wa mikeka yake.

 

Kwa ujumla hadi kufikia sasa Parimatch Tanzania imeshafika takribani mikoa 13 ambapo kuna zaidi ya maduka 29 ya kisasa kabisa yanayotoa huduma za kubashiri.

Na. Mwandishi wetu.

Comments are closed.