The House of Favourite Newspapers

Partey Azua Hofu Arsenal, Kocha Wake Afunguka Mapya

0
Thomas Partey

MIKEL Arteta amefichua kuwa, Thomas Partey anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda baada ya kupata maumivu kidogo siku chache kabla hawajaenda Hispania kucheza na Sevilla.

Juzi Jumanne, Arsenal ilikuwa ugenini nchini Hispania kucheza na Sevilla na kuibuka na ushindi wa mabao 1-2 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Partey ambaye msimu huu amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara, hakuwepo katika mchezo huo jambo lililozua maswali mengi.

Akimzungumzia kiungo huyo, Arteta alisema: “Thomas alipata jeraha mazoezini, hatujui ukubwa wake. Kwa bahati mbaya tunamkosa uwanjani.”

Partey amekuwa akiuguza jeraha la paja wiki za hivi karibuni, lakini aliichezea Ghana mechi zote mbili wakati wa mapumziko ya kimataifa na alikuwa kwenye benchi dhidi ya Chelsea wikendi iliyopita.

ORUMA AILAUMU SIMBA KUMKOSA MAX – AICHAMBUA DERBY -AWATAJA CHAMA na SAIDO WATAKAVYOKOSESHA UBINGWA..

Leave A Reply