The House of Favourite Newspapers

Paul Makonda Aongoza Kumzika Bi Sarah Kibonde Dar (Picha + Video)

Muonekano wa Kaburi la Mke wa Kibonde, Bi Sarah Kibonde baada ya mazishi kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar
Mtangazaji wa Clouds Media, Ephraim Kibonde akiweka shada la ua katika kaburi la mke wake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (shati la kijani) akimsalimia Kibonde kabla ya kuweka taji katika kaburi la mkewe.

Makonda akielekea kuweka taji kaburini.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Greyson Msigwa akiweka taji katika kaburi la mke wa Kibonde kwa niaba ya Ofisi ya Rais Ikulu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akielekea kuweka taji kwenye kaburi.
Sophia Mjema akiweka taji kwenye kaburi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga akimsalimia Kibonde kabla ya kuweka taji kaburini.
Makonda akiwa katikati ya umati wa watu wakati wa mazishi.
Watoto wa marehemu wakimuaga mama yao.
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydee (katikati) akiwa na mumewe wakati wa kuaga nyumbani kwa Kibonde.

MKE wa Mtangazaji wa Clouds Media, Ephraim Kibonde, Bi Sarah Kibonde, amezikwa leo katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo watu mbalimbali walihudhuria akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Greyson Msigwa, wasanii wakiongozwa na Lady Jaydee, wafanyakazi wa Clouds Media Group, ndugu, jamaa na marafiki.

(PICHA: HILALY DAUDI | GLOBAL TV – GPL)

 

Comments are closed.