The House of Favourite Newspapers

Paul Makonda Atembelea Mradi wa Ujenzi wa CCM wa nyumba 6 Jijini Mwanza

0

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda ametembelea Mradi wa Ujenzi wa CCM wa nyumba 6 (full furnished appartiments) ambapo kati yake 4 ni za chini na 2 za ghorofa moja moja uliyopo jirani na Ikulu ndogo ya Jijini Mwanza.

Mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu kiasi cha Tsh Milion 687 ambapo vyanzo vya fedha ni mapato ya ndani ya CCM Mkoa, Wanachama , Wadau na Wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi na hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 41%.

Mwenezi Makonda akiwa hapo, ameahidi kuleta lifti kwaajli ya kuwekwa kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza yenye ghorofa 5.

Aidha, Mwenezi Makonda amesema kwakuwa yeye ni Mwenyekiti na RC Makalla ni Mhasibu katika ujenzi huo, hivyo wataandaa hafla ya chakula cha pamoja ambapo kupitia kadi za mwaliko katika hafla hiyo utawekwa wito wa kuchangia ujenzi wa kumalizia nyumba mradi huo.

“Chama kikiwa na uwezo wa kiuchumi heshima yake inakuwa kubwa, wakati mwingine tunapata Viongozi wala rushwa kwasababu walianza kuweka hela zao taratibu taratibu mwisho wa siku unashangaa Katibu yupo mifukoni mwa mtu kila likija jambo kanuni inapindishwa kwahiyo ni lazima tuwe na uchumi wetu wenyewe ili tujitegemee wenyewe” Alisema Mwenezi Makonda.

Leave A Reply