The House of Favourite Newspapers

Pedi, Pampas, Zamgusa Bashe, Aishauri Serikali – Video

MBUNGE  wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe,  ameishauri Serikali ya Tanzania kuruhusu wakulima wa pamba kuuza moja kwa moja zao hilo kwa wanunuzi ili kuwapunguzia gharama za usafirishaji.

 

Vilevile ameishauri serikali kuzipitia upya kodi na bei za taulo za wanawake na watoto ili kuweza kutoa nafuu kwa wanaozihitaji.

 

Bashe alisema hayo jana Jumatano Juni 25 2019, alipokuwa akichangia Muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka wa Fedha 2019.

 

Alisema hadi hivi sasa hakuna wanunuzi wa pamba katika mikoa ambayo wanalima pamba.

Bashe alisema Serikali ya Tanzania imetoa bei elekezi kwa zao hilo ambayo ni Sh1,200 kwa kilo moja lakini bei ya pamba inategemea soko la dunia.

 

Alisema utaratibu uliowekwa ni wakulima kupeleka pamba katika Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) na hivyo kumlazimu mnunuzi kugharamia usafiri wa kupeleka katika kiwanda.

Alisema ukichanganya na ushuru na kodi anazotozwa mnunuzi inamfanya kununua kwa zaidi ya Sh1,200 kwa kilo.

 

Msikie Bashe akifunguka zaidi katika  video iliyoko chini.

MSIKIE BASHE AKIZUNGUMZA

Comments are closed.