The House of Favourite Newspapers

Penzi la Nandy, Billnass Utajua Hujui

0

UTAJUA hujui! Ndivyo walivyosikika mashabiki baada ya kuwaona wapenzi ambao ni mastaa wa Bongo FLeva, Faustina Charles ‘Nandy’ na William Lyimo almaarufu Billnass wakikumbatiana na kuoneshana kwa mara ya kwanza tangu mwaka huu umeanza.


Pamoja na kuwepo kwa
maneno mengi juu ya kuachana kwao, kumbe wenyewe hawajaachana buana.Usiku wa kuamkia jana, Jumapili, wawili hao ambao ni wachumba wa muda mrefu walimaliza uvumi wa kuachana kwao baada ya Billnass kupanda stejini kwenye tamasha la mwanadada huyo la Nandy Festival na kuonesha mabaha kama yote.

Mpango mzima ulikuwa kwenye shoo hiyo iliyochukua nafasi kwenye Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar na kuacha historia ya aina yake.

 

Maswali yalikuwa mengi tangu Nandy Festival 2021 inaanza kwenye mikoa mbalimbali kabla ya kufikia kilele chake wikiendi iliyopita, yakiuliza yuko wapi Billnass au Nenga?Hata hivyo, kupitia shoo hiyo, Nandy sasa amemaliza sintofahamu hiyo baada ya kutoa majibu kwamba, bado wapowapo sana!

 

Akizungumzia uhusiano wao mara baada ya shoo hiyo, Nandy anasema kuwa, mashabiki wanapenda kuwaona pamoja na hilo walilitimiza na kuwafanya wakawa na furaha.

“Tunakubalika na mashabiki wanapenda sana kutuona na hilo tumelitimiza kwa sababu mashabiki wanapenda sana kutuona wawili,” anasema Nandy.Pia alimshukuru mno Billnass kwa kuja kwenye shoo yake na kwamba ametisha mno.

 

Katika hatua nyingine, Nandy au The African Princess ametajwa kuwa ndiye malkia wa shoo Bongo kwa sasa.Ameweka historia nyingine katika maisha yake ambapo tamasha lake hilo limeweza kujaza viwanja hivyo vya Posta.

Inakadiriwa mpaka kufika saa tano usiku kulikuwa hakuna pa kutema hata mate kwa namna viwanja hivyo vilivyofurika watu.

 

Nandy anakuwa msanii wa kwanza wa kike kuonesha umma kwamba wanawake nao wanaweza kwenye sekta ya burudani.Wasanii wengine waliotisha kwenye shoo hiyo ni pamoja na Jux, Marioo, Baba Levo, Linah, Rosa Ree na wengine wengi ambapo Nandy amesema kuwa, alitaka shoo iyo iwe ya kizalendo zaidi ndiyo maana akawapa nafasi wasanii wengi wa Kibongo.

Leave A Reply