The House of Favourite Newspapers

‘Pepo’ la MASANJA Lazua Balaa Campus Night – Video

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili ambaye pia ni mchungaji, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji, usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Novemba 16, 2019, amewavunja watu mbavu baada kutumia kipaji chake cha uchekeshaji kuwasilisha neno la Mungu kwa wanafunzi waliofika katika Viwanja vya Tanganyika Packers kushuhudia Tamasha la Victory Campus Night.

 

Akizungumza wakati wa Kongamano hilo, Masanja amesema; “Kuna watu bado mpo chuo na mnachanganya imani na matendo (akimaanisha mapenzi), halafu upo mwaka wa kwanza na unamiliki smartphone, wanafunzi msikimbilie mapenzi, kama umeenda chuo bukua kabisa….. Hayo mengine siyo yako… Kazi yako iliyokupeleka hapo ni kusoma.”

 

Kabla ya maneno hayo, Masanja aliingia stejini na wimbo wake maarufu wa KEMEA PEPO ambao uliamsha hisia za mashabiki wote uwanjani hapo na kuanza kucheza kwa furaha sambambamba na msanii huyo ambaye pia hufanya maigizo ya vichekesho.

 

TAZAMA MASANJA HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.