The House of Favourite Newspapers

Petit Man Aifagilia Runinga Mpya ya Shemeji Yake Diamond Kutoka Lampard Electronics

0

PETIT Man akizungumza kwenye uzinduzi wa duka hilo kulia ni mdau wa duka hilo Issa Azam na kushoto ni balozi wa duka hilo Philbertha Athuman.

 

 

STAA wa Bongo, Petit Man amemfagilia hadharani shemeji, msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platniumz’ Dangote baada ya kununua runinga yenye ukubwa wa nchi 100 na ubora wa hali ya juu kutoka duka la Lampard Electronics.

Issa Azam akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo, kulia ni mhamasishaji Snash Snash.

 

 

Petit Man ambaye ni mzazi mwenzake Esma Platniumz ambaye ni dada wa Dangote alisema hayo kwenye uzinduzi wa duka hilo lililopo kwenye Jengo la Klabu ya Simba mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, Dar ambalo linauza bidhaa mbalimbali za umeme kama vile runinga zenye ukubwa tofauti, mashine za kufulia na kukakusha nguo, mafriji na bidhaa nyinginezo.

Mambo yakiendelea dukani hapo.

 

 

Akizungumza na wanahabari Petit Man aliyekuwa na Issa Azam kila mmoja alitumia nafasi hiyo kuelezea ubora wa bidhaa zinazopatikana kwenye duka hilo pamoja na runinga kama hizo.

Muonekano wa nje.

 

 

Upande wake Issa Azam alisema mteja atakayenunua runinga kama hiyo dukani hapo atakwenda kufungiwa kwake na mafundi wataalamu kutoka dukani hapo.

Leave A Reply