The House of Favourite Newspapers

Fahamu Maajabu ya Infinix NOTE 11, Kioo cha Amoled

0

Siku hadi siku tumekuwa tukishuhudia namna makampuni ya simu yanavyochuana kuleta simu zenye sifa za hali ya juu na moja ya kampuni hizo yenye kuonekana kuja kwa kasi ni kampuni ya simu Infinix.

 

Habari zilizopo mitandaoni ni kuwa Infinix kuja na simu ya kwanza kutoka kwenye series ya NOTE yenye kioo aina ya AMOLED na kusemekana Infinix NOTE 11 ni simu ambayo itakuwa ikitumia chaji kwa udogo zaidi.

 

Sifa za kioo cha AMOLED ya NOTE 11

  • chenye kusifika kutokana na ulaji mdogo wa chaji ukilinganisha na vioo vyengine kama IPS.
  • Smooth/ kinateleza kwa haraka wakati wa kuperuzi.
  • Rangi za picha zinazotokana na simu yenye kioo cha AMOLED hushabihiana na mazingira halisi.

Sifa nyengine ni kuhusu muonekano wa simu hiyo, inasemekana Infinix NOTE 11 kuja kuwa simu ya kwanza yenye umbo jembamba zaidi lililotawaliwa na wigo mpana wa kioo cha inch 6.7fhd kuwahi kuwepo kwenye series ya NOTE.

 

Hizi ni baadhi ya dondoo ambazo zimeonekana kuzagaa kwenye mitandao mbalimbali ya tech kama Tanzaniatech na nyenginezo. Je, unaisi ni feature gani nyengine mpya kuja na Note 11 https://bit.ly/3BHedZw?

Tafadhali kaa karibu na @infinixmobiletz kujua zaidi kuhusu simu hii.

Leave A Reply