The House of Favourite Newspapers

Pialali Kuzichapa na Muhindi Bagamoyo

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Shiva Gurgaon raia wa India katika pambano la  ubingwa wa International UBO linalotarajia kupigwa  Desemba 16, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Travel Lodge, Bagamoyo mkoani Pwani.

 

Pialali ambaye pia anashikilia Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati  ambao aliupata  Julai 23, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live kufuatia kumchakaza  vikali mpinzani wake, Rigen Champion  raia wa DR Congo.

 

Mbali ya pambano hilo lililoandaliwa na Sharif Promotion ambalo limedhaminiwa na Kinite Castle, Travel Lodge, mapambano mengine ya utangulizi yatakuwa ni kati bondia Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe, dhidi ya Ambukile Chusa (raundi kumi), Saleh  Mkalekwa dhidi ya Hamis Ng’onda (raundi nane).  

 

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni  Bruno Vifua viwili dhidi ya  Said Uwigo (raundi nane) wakati Ramadhani Mchongo akitarajia kuzichapa  na Twalip Tuwa huku  mwanadada,  Rehema Nakozi atazitwanga na Happy Daudi  (raundi sita)  na Pallasoguru Mchalinze dhidi ya Shebi Chui  (raundi kumi)

Comments are closed.