The House of Favourite Newspapers

PICAHZ: Wakazi wa Mkuranga Waikomalia Droo ya Pili ya Shinda Nyumba

Mr. Shinda Nyumba akiwasaidia wasomaji kujaza kuponi za Shinda Nyumba.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Keffa akimsadia msomaji kujaza kuponi.

Wasomaji wakichangamkia magazeti ya Global Publishers ili wajaze kuponi za shinda nyumba na kujaribu bahati yao.

Msomaji akichana kuponi na kuiweka kwenye chombo maalum baada ya kuijaza.

Wasomaji wakichangamkia gazeti la Risasi na Championi.

Ni mwendo wa kujaza kuponi za Shinda Nyumba.

Msomaji akikabidhi kuponi ya Shinda Nyumba baada ya kuijaza.

Mr. Shinda Nyumba akimsaidia mama kujaza kuponi.

PICHA NA MUSA MATEJA

LEO wakazi wa Mkuranga mkoani Pwani wamechangamkia vilivyo magazeti ya Risasi na Championi yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers inayoendesha shindano kabambe la Shinda Nyumba ambapo mshindi kwenye droo kubwa atajishindia nyumba na fenicha zake ndani.

Katika shindano hilo, droo ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba awamu ya pili itafanyika Machi 17 mwaka huu ambapo kama ilivyokuwa ile ya kwanza, itatawaliwa na zawadi kibao zitakazobadili maisha ya washindi.

Droo ndogo ya kwanza ilifanyika Februari 8 mwaka huu katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakheem ambako washindi watano walijishindia zawadi za pikipiki, televisheni, simu za kisasa, vyombo vya jikoni na vitu vingine vingi. Washindi hao walikuwa ni Andrew Mtunguja wa Muheza mkoani Tanga, Ambrosi Ligonja wa Mang’ula, Morogoro, Evans Stanley wa Kunduchi, Said Mohamed na Gasto Peter wote wa Kimara jijini Dar es Salaam.

Ndani ya magazeti ya Global Publishers ambayo ni Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko, Amani na Championi, kwenye ukurasa wa pili kuna kuponi ambayo unaijaza na kuileta kuponi hiyo kwenye ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar au unaweza kupeleka kwa mawakala au wauza magazeti wenye ndoo maalumu za Shinda Nyumba, ambao wako nchi nzima.

Comments are closed.