The House of Favourite Newspapers

Picha 5: Wabunge Chadema Walivyotaka Kumchapa Makonde Mbunge wa CCM

0

 

MBUNGE wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza, jana alizua timbwili nje ya viwanja vya bunge na kunusurika kupigwa na wabunge wa upinzani kutokana na kuwatambia kwamba atahakikisha Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye yuko kifungoni anaendelea kusota huko.

 

Wabunge sita wa Chadema usiku wa kumkia leo wamehojiwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia mbunge huyo.

 

 

Mwenyekiti mwenza wa wabunge wanaounda umoja wa katiba (Ukawa) James Mbatia amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga, Saed Kubenea(Ubungo), Pauline Gekul (Babati Mjini), Frank Mwakajoka (Tunduma), Joseph Selasini (Rombo) na Cecilia Pareso (Viti Maalum).

 

 

 

Leave A Reply