The House of Favourite Newspapers

Kumbe Dola Milioni 20 Kwa Kanye Hazikuwa Zawadi!

0

SI KWELI! Huku bifu la wanamuziki wawili, Jay Z na Kanye West likiendelea, kulikuwa na taarifa za chinichini zikisema kwamba zile dola milioni 20 zaidi ya bilioni 40 alizopewa Kanye West zilikuwa kama zawadi kwa ajili ya kugharamia gharaza za ziara yake kitu ambacho upande wa pili umekana kwa nguvu zote.

Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na Kanye West viliweka wazi kwamba pesa hizo zilikuwa ni makubaliano ambayo yaliandikwa katika mkataba na hazikuwa kama zawadi hivyo Tidal kutoa kiasi hicho ilikuwa ni lazima.

Kama utakuwa unakumbuka, katika albamu ya Jay Z ya 4:44 kwenye Ngoma ya Kill Jay Z mseela aliimba “But you got hurt because you did cool by ‘Ye // You gave him 20 million without blinkin’ // He gave you      20 minutes on stage, f*** was he thinkin’? // ‘F*** wrong with everybody?’ is what you sayin’ // But if          everybody’s crazy, you’re the one that’s insane.”  

Na: Nyemo Chilongani, (GPL)

Leave A Reply