The House of Favourite Newspapers

PICHA: Muonekano wa Ndani wa Gari Lililomteka Mo Dewji

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amezungumzia tukio la kupatikana kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji kutoka kwenye mikono ya watekaji na kusema imebainika nia ya watekaji hao walitaka awapatie pesa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2018, Sirro amesema; “Nimeambiwa kwamba waliomteka Mohammed Dewji amesema walimwambia walitaka pesa, alipowauliza shilingi ngapi hawakusema, aliwapa simu waongee na baba yake lakini waliogopa kwa sababu wanafahamu ulinzi wetu ni imara tungewakamata.

“Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana, baada ya kuona hawawezi kutoka, njia pekee ni kuliacha hili gari hapa majira ya saa saba usiku, MO aliwapa taarifa wazazi wake wakaja kumchukua.

Comments are closed.