The House of Favourite Newspapers

Picha za Utupu na Young D, Amber Lulu Afikishwa Polisi

0
Amber Lulu na Young D.

MUUZA sura maarufu kwenye video za Bongo, ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu jana Jumanne alikamatwa na kupelekwa kwenye Kituo cha Polisi Urafiki jijini Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu kusambaa mitandaoni kwa picha alizopiga akiwa utupu pamoja na mwanamuziki mwenzie, Young D.

Amber Lulu alihojiwa kwenye kituo hicho na kuachiwa saa chache baadaye baada ya kukamilisha kutoa maelezo aliyotakiwa.

Juhudi za kumtafuta Aber kwa ajili ya kutoa taarifa ya tukio hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokewi kwa muda wote tuliompigia.

Tukio hili la kuhojiwa na polisi limetokea baada kusambaa kwa picha iliyozua gumzo kubwa la kimaadili inayomwonesha Amber akiwa ameziba matiti kwa kutumia mikono tu akiwa amevaa nguo ya ndani aina ya bikini pekee huku Mwanamuziki Young D akikodolea macho makalio ya mwanadada huyo.

 

Kimenuka! Amber Lulu Amwaga Machozi Akimtuhumu Young D Kuvujisha Picha Yao ya Utupu Mitandaoni

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply