The House of Favourite Newspapers

Nyumba Yateketea kwa Moto Magomeni Dar (Video)

0
Nyumba moja iliyopo Magomeni Makanya jijini Dar wanayoishi wanafamilia na wapangaji ikiendelea kuteketea kwa moto.
Wapangaji wa nyumba iliyoungua wakiwa na wananchi wengine baada ya kuuzima moto eneo la Magomeni Makanya jijini Dar.
Wananchi wakiendelea kushangaa nyumba hiyo.
Mwananchi akihojiwa na Global TV Online kuhusu moto huo.
Wananchi wakiendelea kuongea na Global TV.

Nyumba moja iliyopo Magomeni Makanya jijini Dar wanayoishi wanafamilia na wapangaji leo imeteketea kwa moto ambapo wenyewe wakidaiwa kuwa kwenye msiba Mbezi jijini. Taarifa  zilizopatikana eneo la tukio zilidai kuwa nyumba hiyo ilianza kuonekana ikiungua kunako saa nne asubuhi chanzo chake kikidaiwa kuwa hitilafu ya umeme.

Mwandishi wetu akiwa eneo la tukio aliwakuta askari wa kikosi cha Zimamoto wakiendelea kuuzima moto huo huku askari polisi wenye silaha wakilinda usalama eneo hilo hasa kudhibiti vibaka.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL  

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply