The House of Favourite Newspapers

Picha za Wema, Bwana’ke Wakiwa Bafuni Zavuja

0

DAR ES SALAAM: MREMBO mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ ameendelea ‘ku-shine’, safari hii zimevuja picha mpya akiwa bafuni na mpenzi wake aitwaye Bakari Kila.

Chanzo makini kilinyetisha kuwa, licha ya Bakari kuwa nyuma ya nondo kwa msala wa madawa ya kulevya Mombasa, nchini Kenya, bado ana ubuyu wa picha mpya za Wema wakioneshana mahaba na mpenzi wake huyo wakiwa bafuni.

“Achana na skendo ya unga inayomtafuna bwana wa Wema, sahau kabisa kuhusu zile picha zilizovuja Wema akiwa na Bakari, mimi ninazo picha nyingine mpya wakiwa bafuni.

“Yani ni full mahaba, Wema anaonekana akiwa ametinga kanga moko (moja), amemkumbatia Bakari huku akimpiga busu motomoto,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kuna moja Wema anambusu Bakari shavuni lakini kuna nyingine anambusu mdomoni kabisa kama njiwa vile tena wakiwa kwenye hisia kali za kimalovee. Madam hana habari tena yeye inaonesha ndiye aliyekuwa anapiga picha.”

Baada ya kuzitia kibindoni picha hizo, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Madam ili kuweza kumsikia anazizungumziaje picha hizo zinazomuonesha akiwa amezama kwenye ulimwengu wa kimahaba lakini hadi tunakwenda mitamboni, simu yake haikupokelewa.

Bakari anatajwa kuwa na mkwanja mrefu kiasi cha kumtuliza Wema hadi akaacha ‘makeke’ ya mjini, kabla jamaa huyo hajataitiwa kwa madawa ya kulevya nchini Kenya.

Stori: Erick Evarist, Ijumaa WIKIENDA.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

Leave A Reply