The House of Favourite Newspapers

Picha za x zatikisa ndoa ya kigogo!

1

IMG-20151126-WA0015

Aibu ilioje! Picha chafu za ngono ‘X’ za mrembo aliyetajwa kwa jina moja la Mariam, mkazi wa Kinondoni jijini Dar, zinadaiwa kuitikisha ndoa ya kigogo wa sekta nyeti ya fedha baada ya kunaswa kwenye simu yake na mkewe aliyetambulika kwa jina moja la Aneth, wote wakazi wa jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Aneth, picha hizo zimeacha mpasuko mkubwa kwenye ndoa yao kwa kuwa mara nyingi amekuwa akimhisi mumewe kutokuwa mwaminifu huku safari za Dar zikiwa hazikauki.

Alisema kuwa, amekuwa akifuma meseji za kimapenzi kwenye simu ya mumewe hivyo kuchukua namba za simu za mtumaji kisha kumtafuta mhusika ndipo alipogundua ni huyo Mariam baada ya kumpigia kwa lengo la kumuonya.

“Ni muda mrefu sana nimekuwa nikimshtukia mume wangu, lakini amekuwa mbishi na mbabe kupindukia hali ambayo imekuwa ikizua ugomvi mkubwa kati yetu, mbaya zaidi nimekuwa nikikuta meseji za kimapenzi kutoka kwa huyo Mariam, picha zao wakiwa katika mahaba mazito, lakini nilipomtafuta mhusika (Mariam) aliishia kunitishia kwa maneno makali,” alisema Aneth.

Baada ya kumalizana na mke, mwandishi wetu alimtafuta Mariam kupitia namba ya simu alizopewa na Aneth (mwenye mume) ambapo aliposomewa tuhuma hizo, alikiri kuwa picha ni zake lakini alizituma kwa mwanaume huyo kwa bahati mbaya na kwamba alishazungumza na Aneth ambao kwa pamoja waliyamaliza.

“Jamani nilishazungumza na Aneth, tukayamaliza lakini kama mtatoa picha hizo gazetini, sitaanguka peke yangu, nitateketea na mumewe, mimi ndiye Mariam, mwingine feki, kutembea na mume wa mtu siyo kosa la jinai, wala haliko kwenye katiba,” alisema Mariam huku sauti yake ikirekodiwa kwenye kifaa maalum cha kunasa sauti.

1 Comment
  1. Hakikah says

    Kimdoxho moa ama nn*

Leave A Reply