The House of Favourite Newspapers

Zimamoto Yajibu Tuhuma za Kuchelewa Matukio ya Moto

JESHI la Zimamoto nchini kupitia kwa Kamanda Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Kitaalam (SDA) wa Jeshi la Zimamoto Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja limejibu tuhuma ambazo limekuwa likilalamikiwa kuhusu kuchelewa kufika kwenye maeneno ya matukio mara baada kuarifiwa kuwa kuna moto unawaka.

Mkaguzi Joseph Mwasabeja.

Akijibu swali la Mwandishi wa habari wa Global Publishers ambako alitembelea leo wakati wa Mahojiano Maalum na Global TV Online, Mwasabeja amesema kuwa tatizo kubwa limekuwa ni miundombinu mibovu ya barabara na ujenzi holela usio na mipango kwenye baadhi ya maeneo hivyo kuwafanya kushindwa kufika kwa wakati.

Kuhusu kufika bila maji, amesema kuwa magari ya Zimamoto yana uwezo wa kubeba maji yenye ujazo hadi lita 5,000 ndipo linaweza kukimbia kwa kasi na kuwahi eneo la tukio tofauti na likiwa na mzigo mkubwa.

“Magari yetu yanaweza kubeba hadi lita 5,000 za maji na yakakimbia kwa kasi hivyo kufika haraka eneo la tukio tofauti na tunapobeba mzigo mkubwa wa maji. Kulingana na uwezo wa pampu zetu, husukuma hizo lita 5,000 kwa dakika 15 pekee hivyo ikitokea maji yameisha na moto haujazima ndipo tatizo linapotokea,” alisema.

Kuhusu uwezo wa mitambo ya kuzimia maghorofa, amesema kuwa jeshi hilo lina mitambo inayoweza kusimama na kufikia jengo lenye ghorofa 18 na kuzima moto kwenye jengo lenye hadi ghorofa 21.

Mkaguzi Joseph Mwasabeja akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shingongo.

Kuhusu elimu ya kuzima moto ameeleza kuwa tahadhari ya kwanza wakati wa janga la moto ni kuchukua kifaa cha kuzimia moto (fire extinguisher) na kuuzima moto, kuzima main switch ya umeme na kupiga simu Zimamoto kwa namba 114 bure mitandao yote watafika kwa ajili ya kuzima na kuokoa.

Akiwa katika picha ya pamoja na wahariri na waandishi wa Global Publishers.

Kuhusu malipo amesema: “Jeshi hili la Zimamototo ni jeshi la wananchi kama majeshi mengine, hivyo tunamhudumia mwananchi bure bila kumtoza ila wanaotoza pesa ni makampuni binafsi ya Zimamoto.”

Akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Slaeh Ally

Aidha ametoa wito kwa wananchi wasichezee namba ya dharura (emergency call), wapige tu wakati kuna tukio pekee na siyo kwa ajili ya mambo yao binafsi hali ambayo itaifanya namba hiyo iwe huru na kufanya kazi kulingana na madhumuni ya matumizi yake.

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.