The House of Favourite Newspapers

Pichaz: Ukweli Kuhusu Mapambano ya Polisi na Majambazi Vikindu

0

IMG_7766Eneo la Mtaa wa Vikindu Mashariki mkoani Pwani kwenye nyumba ya mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mzee Manitu paligeuka uwanja wa mapambano baada ya polisi kuizingira nyumba hiyo na kupiga risasi nyingi hewani wakati wakimtaka jambazi anayetuhumiwa kufanya mauaji ya katika tukio la kuuawa askari polisi wanne waliokuwa wakibadilishana lindo kwenye Benki ya CRDB Tawi la Mbande wialayani Temeke jijini Dar. Katika tukio hilo Afisa wa Polisi mwenye cheo cha ASP Thomas Njuki wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi ameuawa.

IMG_7779Baada ya jambazi huyo kumuua askari, jeshi la polisi liliongeza nguvu eneo hilo na kupiga mabomu na risasi nyingi hewani zilisababisha taharuki katika eneo hilo na kusababisha kila mmoja aseme lake.

IMG_7795Mapaparazi wetu baada ya kufika eneo hilo walitaka kuzungumzia na maofisa wa polisi waliokuwa eneo hilo akiwemo, RPC wa Pwani, Bonaventura Mushongi, Gilles na Kamishna Mwandamizi wa Jeshi hilo, Liberatus Sabas lakini wote walisema hawawezi kuongea chochote mpaka wapate ruhusa kutoka ngazi za juu kwa kuwa tukio hilo si la Kimkoa bali ni la Kitaifa.

IMG_7814Licha ya viongozi hao kukataa kuzungumza, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili ambaye alikuwa bega kwa bega na askari hao alisema kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wanaume 7 ambapo walikutwa wanaume 3 na wanawake 3 ambapo mwanaume mmoja aliyetajwa kumuua Afisa huyo wa Polisi alitoroka pamoja na silaha yake.

IMG_7818Hakuna Jambazi yeyote aliyeuawa katika tukio hilo zaidi ya afisa huyo wa polisi.

Mwenkiti wa serikali ya Mtaa Mohammed IsmailMwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili

Angalia picha
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ ISSA MNALLY /GPL.

Leave A Reply