The House of Favourite Newspapers

Mkutano wa Vyama vya Siasa Wapigwa Kalenda Hadi Sept 3-4

0

Vyama vya Siasa (1)

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungia akisisitiza juu ya umuhimu wa mkutano wa vyama vya siasa utaofanyika Septemba 3 hadi 4 kwaka huu jijini Dar es Salaam mkutano uliofanyika katika Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam.

Vyama vya Siasa (2)

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Vuai Ali Vuai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kusogeza mkutano wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya baraza la vyama vya siasa, Constatine Akitanda.

BARAZA la vyama vya Siasa nchini limesogeza mbele mkutano wa kujadili sintofahamu iliyojitoeza kwa baadhi ya vyama vya siasa na kusababisha kuwepo kwa hofu, na taharuki kwa wananchi.

Mkutano huo ulitangazwa kufanyika Agosti 29 hadi 30 na kusogezwa kufanyika Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Vuai Ali Vuai amesema kusogeza mbele kwa mkutano huo kumetokana na kutaka kutoa muda kwa wadau ili waweze kujiandaa.

Amesema kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwa wadau kukutana na kujadili mambo yaliyojitokeza na kuweka sawa kwa mstakabali wa taifa.

Jukwaa la viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadiliana masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa nchini kwetu.

Amsema kila chama cha siasa kinawakilishwa na viongozi wawili wa ngazi kitaifa katika Baraza la Vyama vya Siasa, ambapo kiongozi mmoja anapaswa kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar.

Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Baraza huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Baraza la Vyama vya linaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za zilizotungwa na Baraza.

Baraza la vyama vya siasa lina majukumu ya  kuishauri msajili wa vyama vya siasa kuhusu migogoro baina ya vyama vya siasa,kumshauri Msajili wa vyama vya siasa kuhusu masuala yenye masilahi ya kitaifa yanayohusu vyama vya siasa na hali ya siasa nchini.

Aidha amesema kazi ya baraza hilo kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa,kushauri kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.

Baraza hilo linaweza kumtaarifu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala yoyote yanayohusu utendaji wa chama chochote cha siasaKamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti wa Baraza, Makamu Mwenyekiti wa Baraza, wenyeviti wa kamati nne za Baraza na katibu wa Baraza.

CREDIT: MICHUZI BLOG

Leave A Reply