The House of Favourite Newspapers

Pichaz + Video: Dokii Ajitofautisha Na Waigizaji Wenzake!

0
Staa wa maigizo na filamu za kicheshi Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’.

STAA wa maigizo na filamu za kicheshi Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amejitofautisha na wasanii wenzake, ambapo pamoja na mambo mengine amesema yeye si miongoni mwa waigizaji wanaotumia pesa zao nyingi katika mambo yasiyokuwa na tija, ikiwemo kiubadili magari pasipokuwa na sababu maalum, jambo ambalo amedai kamwe hawezi  kulifanya.

Katika mahojiano maalum na Global TV Online mapema leo, msanii huyo mwenye kujulikana zaidi kama Mkenya kutokana na umahiri wake wa kuigiza sauti za watu wan chi hiyo, alisema yeye ni mfanyabiashara kabla hata hajajiingiza kwenye masuala ya uigizaji, hivyo anaiheshimu pesa, kwamba huenda wasanii wanaobadilisha magari kila mara, wanakuwa na pesa zisizokuwa na kazi maalum, lakini kwa upande wake, kila pesa inayoingia mfukoni inakuwa na mahesabu makali.

“Mimi ni mfanyabiashara ujue, tena nilianza kabla hata sijawa muigizaji kwa hiyo naijua na kuiheshimu sana chapa (pesa), hao wasanii wengie wanaobadilisha magari, labda wana pesa za ziada zisizokuwa na kazi maalum ndiyo maana wanafanya hivyo, lakini mimi kama mtu wa bgiashara, hata nikibaki na gari moja sioni kama kuna shida juu ya hilo,” alisema Dokii.

Mfanyakazi wa Global TV na Global, Brighton Masalu (kulia) akimueleza jambo Dokii.

Kwa kufaidi zaidi mahojiano hayo na Dokii, usikose kutembelea Global TV Online, kwa kufungua YouTube kisha kuandika neno Global TV Online na hapo utaweza kujionea moja kwa moja mahojiano na Dokii.

(Habari: Brighton Masalu/GPL)

Leave A Reply