The House of Favourite Newspapers

PICHAZ: Watoto wa Lucky Vincent Walivyopokelewa KIA

0
Mtoto Doreen akishuka kwenye ndege.

 

WATOTO watatu wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliokuwa majeruhi wa ajali iliyotokea Karatu na kwenda kutibiwa nchini Marekani, tayari wamewasili leo asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Moshi na kupokelewa na mamia ya Watanzania.

Doreen na Wilson wakipokelewa na kukabidhiwa maua kama ishara ya upendo kwao.

 

Doreen, Sadia na Wilson walikuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy, Sioux City nchini Marekani wamewasili kwa ndege ya Samaritan’s Purse wakitokea nchini humo baada ya kupata nafuu. Wametua Tanzania wakiwa wenye furaha na faraja kubwa.

…Wakiwa kwenye hafla fupi ya kuwapokea.

Mamia ya wakazi wa Arusha, wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, wanafunzi wenzao na viongozi mbalimbali wa serikali wamefika kwa ajili ya kuwapokea watoto hao. Baadhi ya viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mbunge Lazaro  Nyarandu makatibu tarafa wa mikoa na viongozi wa wilaya za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Wametua nchini wakiwa na wazazi wao, madaktari na watalii waliowaokoa siku ya tukio ikiwa ni jumla ya wajumbe 16.

Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.

Mtandao wa Global Publishers unawashukuru madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea na kuchangia chochote kusaidia matibabu ya watoto hao.

 

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Full Video: Ndege Iliyowabeba Watoto wa Lucky Vincent Ikitua Kutoka Marekani

Leave A Reply