MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeiahirisha tena kesi inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu na wenzake wawili kwa madai ya kuwa haijakamikisha kuandaa uamuzi wa kupokea au kutopokea kielelezo cha msokoto na vipisi vya bangi.
Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar wakati kesi ikiunguruma, Hakimu Thomas Simba amewaambia mawakili wa serikali na utetezi kuwa hajamaliza kuandaa uamuzi huo kutokana na kazi nyingi kumkabili na hivyo akaiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 31 mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi pia alisema Septemba 12 na 13 itaanza kusikilizwa.
NA DENIS MTIMA/GPL