The House of Favourite Newspapers

Pierre Liquid Amrudisha Makambo Yanga – Video

0

MCHEKESHAJI maarufu wa kwenye mitandao hapa nchini, Peter Mollel ‘Pierre Liquid’ ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Yanga, amesema kwa jinsi anavyomkubali mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Heritier Makambo, anatamani kumrudisha fasta ndani ya kikosi hicho ili arudishe furaha.

 

Jana Jumatano, Pierre alitembelea Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori jijini Dar, kisha kufanya mahojiano maalum ndani ya kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi.

Baada ya kumaliza mahojiano hayo, akaliambia Spoti Xtra kuwa: “Mimi nina kauyangayanga ndani yangu na kama unavyojua Yanga inaonekana kupata wakati mgumu kwenye safu ya ushambuliaji msimu huu jambo ambalo linanifanya nitamani kumrejesha tena mshambuliaji wetu wa zamani Heritier Makambo ili arejeshe furaha kama ilivyokuwa msimu uliopita.

 

”Msimu uliopita, Makambo raia wa DR Congo, alifunga mabao 17 akiwa na jezi za Yanga katika Ligi Kuu Bara, kabla ya kuondoka na kutua Horoya AC ya Guinea.

 

Ili kusikiliza matangazo ya +255 Global Radio popote ulipo, pakua App ya Gobal Radio katika Android au iOS au ingia www.globalradio.co.tz.

Leave A Reply