The House of Favourite Newspapers

Pigo Jingine Chadema, Katibu wa Chama Wilaya ya Kahama Atimkia CCM

0

KATIBU wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga amejivua uwanachama wa chama hicho na na nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akitangaza uamuzi huo Ndugu Michael Fabian Kigenda katika barua yake ya kujivua uwanachama na kuachia nafasi zake za uongozi ndani ya Chadema amesema haoni haja ya kuendelea kuwa mpinzani na kupingana na serikali ya Rais John Magufuli kwani Rais amekuwa akitekeleza agenda zote ambazo Chadema ilikuwa ikizihubiri na hivyo chama hicho kimekosa agenda kwa sasa.

Leave A Reply