The House of Favourite Newspapers

Pluijm: Kwa Ngoma na Chirwa mbona Ubingwa mapema

BAADA ya uongozi wa Azam hivi karibuni kumtangaza mshambuliaji wao mpya Mzambia, Obrey Chirwa, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm ameibuka na kusema kuwa sasa ubingwa mapema tu.

 

Azam mpaka sasa hawajapoteza mchezo wowote katika ligi kuu wakiwa nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 12, wakishinda 9, wakitoka sare 3 huku wakiwa na pointi 30.

 

Akizunguma na Championi Jumatatu, Pluijm alisema kuwa Chirwa akiungana na Donald Ngoma, watasaidia kutengeneza safu imara zaidi ya ushambuliaji kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Alisema washambuliaji wake hao wawili wanajuana vizuri sana kwani walishafanya kazi pamoja wakiwa Yanga, hivyo kombinesheni yao itakuwa hatari sana kitu ambacho kitasababisha wao kupata ubingwa mapema.

 

“Kila mtu anajua uwezo wao walipokuwa Yanga na hata uwezo wa Chirwa na Ngoma nadhani watu wengi wanaujua kitu ambacho kitaleta kombinesheni nzuri kwani wanajuana vizuri na walishafanya kazi pamoja kitu ambacho kitaunganisha kombinesheni hatari na inaweza kuwa tukapata ubingwa mapema,” alisema Pluijm.

 

IBRAHIM MRESSY, Dar es Salaam

Comments are closed.