The House of Favourite Newspapers

POGBA KAPANIA KWENDA BARCELONA AACHANE NA MOURINHO

Despite captaining Manchester United against Leicester, Paul Pogba still wants to leave

MWANASOKA Mfaransa, Paul Pogba anataka kuondoka  Manchester United ya Uingereza na kwenda Barcelona ya Hispania hata kama ugomvi wake na kocha/meneja wake, Jose Mourinho ukimalizika.

Ili kumpoza mchezaji huyo, Mourinho alimpa ukapteni katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Leicester, hata hivyo, alipoulizwa baada ya mechi alijisikiaje, Pogba alisema asingeweza kujibu chochote kwa kuogopa kwamba angepigwa faini na klabu hiyo.

“Kuna mambo nikiyasema, klabu itaniadhibu kwa kunipiga faini,” alisema.

Imeonekana kwamba lengo kuu la mchezaji huyo ni kuichezea Barcelona, hilo la ugomvi wake na Mourinho ni la pili.Pogba has reportedly agreed terms on a move to Barcelona, but United do not want to sell

Pogba, 25, aliyendoka Man U wakati wa kocha  Sir Alex Ferguson na kwenda Juventus mwaka 2012, amemwambia naibu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo, Ed Woodward na wasaidizi wake kwamba anataka kuondoka.The midfielder starred for France at the 2018 World Cup, netting in the final win over Croatia

Comments are closed.