The House of Favourite Newspapers

Pole Pole Afunguka Maandalizi Ya Mkutano Mkuu wa CCM Kesho -Video

0

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole leo Aprili 29, 2021 amezungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu kuongeza kuwa  wajumbe kutoka sehemu mbalimbali watashiriki mkutano mkuu wa chama hicho kesho jijini Dodoma

 

Amesema pamoja na wajumbe hao ambao watashiriki kupiga kura, wapo wageni 1,000 watakaoshiriki mkutano wakiwamo kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini, wawakilishi wa vyama rafiki vilivyoshiriki katika ukombozi wa Bara la Afrika na mabalozi.

 

Amebainisha kuwa mkutano huo utaongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula na makamu mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

 

Aidha amesema kikao hicho kitatoa mwelekeo wa Taifa kisera kwani itatolewa hutuba ya mwenyekiti mpya wa chama hicho atakayechaguliwa.

 

“Kikao hicho cha mkutano mkuu maalumu chenye jukumu la kupigia kura jina moja litakalowasilishwa ili kumpata mwenyekiti, kinaketi baada kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kukaa leo jijini hapa na kuandaa ajenda za mkutano mkuu maalumu,” amesema Polepole.

Leave A Reply