The House of Favourite Newspapers

Polepole: Chama Chetu Sio Daladala….. Ni Heri Akabaki Hukohuko (Video)

0

BAADA ya Msanii maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu kutangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana Ijumaa, Desemba 1, 2017 kwa kile alichodai kuwa ni kukosa amani ndani ya chama hicho.

Kupitia kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram, Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametuma ujumbe mzito kwa Wema ambaye ni alikuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Tanzania 2006, amekisema, Chama chetu sio Daladala mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote, ni heri akabaki hukohuko ama akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu”

Wakati anatangaza kuhama, Wema alisema Chadema ni kama nyumba inayomkosesha amani hivyo hana haja ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo.Amesisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM.

Alisisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM.

Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu walihamia Chadema mwezi Februari mwaka huu baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Alichokiandika Polepole.

MASTAA WAMFUNGUKIA WEMA ISHU YA KURUDI CCM!

TUJIKUMBUSHE: Wema Sepetu Arudisha Kadi ya CCM na Kujiunga na CHADEMA (Video)

KISA WEMA: Polepole, Steve Nyerere Wavaana Vikali! “Tulia CCM Siyo Yako”

Leave A Reply