The House of Favourite Newspapers

Polisi Wa Nigeria Wakabiliana Na Waandamanaji

0

Jeshi la Polisi nchini Nigeria, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji walioingia barabarani leo katika maandamano ya amani ya kupinga utawala wa rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari.

 

Vurugu kubwa zimezuka kwenye Miji la Lagos na Abuja, wakati polisi wakikabiliana na waandamanaji hao, waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofautitofauti wa kumtaka Rais Buhari ajiuzulu.

 

Awali, jeshi la polisi lilipiga marufuku maandamano hayo, yaliyoandaliwa na asasi mbalimbali za wanaharakati nchini humo, lakini marufuku hiyo imepuuzwa na waandamanaji wanaosisitiza kwamba ni haki yao ya kikatiba kuandamana.

 

Tofauti na maandamano ya End Sars yaliyotingisha nchi hiyo mwaka 2020 na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu, taarifa zinaeleza kwamba leo polisi wamekuwa makini na matumizi ya nguvu kubwa kupita kiasi, ambapo ni mabomu ya machozi pekee ndiyo yanayotumika.

 

Baadhi ya waandamanaji, wengi wakiwa ni vijana, wanaeleza kwamba hawakubaliani na utawala mbaya nchini humo, kukithiri kwa vitendo vya rushwa na kuzorota kwa usalama.

 

Vikosi vya askari kutoka Jeshi la Nigeria, Jeshi la Polisi, Department of State Security na askari wa kikosi maalum cha NSCDC wametawanywa kwa wingi karibu nchi nzima, kukabiliana na maandamano hayo ambayo Jeshi la Polisi ya Nigeria linayaita kuwa haramu.

Leave A Reply