The House of Favourite Newspapers

Polisi Wafungua Jalada Kuchunguza Iwapo Nondo Alitekwa au La! – Video

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limefungua kuchunguza ili kubaini kama ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo alitekwa au alitoa taarifa za uongo.

Nondo, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu usiku wa kuamkia jana na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK” (niko hatarini) ambapo amepatikana akiwa ametupwa barabarani Mafinga mkoani Iringa na baada ya kuzinduka, imeelezwa alijikokota na kuelekea Kituo cha Polisi Mafinga kuripoti.

 

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire, amesema Nondo amepatikana akiwa salama bila jeraha lolote wala kupigwa lakini wamefungua jalada hilo kwa ajili ya uchunguzi na mpaka sasa bado yupo kituoni hapo na iwapo atabainika alidanganya atashughulikiwa kama wahalifu wengine.

 

ABDUL NONDO APATIKANA AKIWA HAI IRINGA, POLISI WAMCHUNGUZA!

Comments are closed.