Jeshi la Polisi Lafunguka Sababu ya Kumshikilia Kada wa Chadema Twaha Mwaipaya – Video
JESHI la polisi mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi dhidi ya mratibu wa hamasa wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Twaha Mwaipaya anayetuhumiwa kutoa taarifa za uongo katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu kupanda kwa gharama za umeme wakati akijua kuwa yeye sio msemaji wa shirika la umeme nchini TANESCO na kuzua taharuki.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma ACP Martin Otieno amesema baada ya kukamilika kwa uchunguzi wanatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote.