The House of Favourite Newspapers

Polisi Wafunguka Tukio La Mtoto Mwenye Ulemavu Wa Ngozi Kukatwakatwa Na Panga – Video

0


Mtoto Kazungu Julius (10) Mkazi wa Mtaa wa Mtakuja Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro Wilayani Geita Mkoani Geita, amejeruhiwa kwa kukatwa na Panga sehemu Mbalimbali za mwili wake na Mtu asiyejulika kisha kutokomea kusikojulikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita , Kamishina Msaidizi Mwandamizi SACP Safia Jongo amesema siku ya Mei 4 Mwaka huu Majira ya Saa mbili usiku mtoto huyo aliagizwa na Mama yake wakati anatoka nje ya nyumba kuna mtu alikuwa amejificha sura yake na kuanza kumchana chana Mapanga sehemu za Mwili wake.

Leave A Reply