The House of Favourite Newspapers

Polisi wamfungia kazi Dk. Mwaka!

0

mwaka223Tabibu Juma Mwaka ‘Dk. Mwaka’

MWANDISHI WETU, WIKIENDA

DAR ES SALAAM: Mara tu baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangallah kumpa saa 24 mmiliki wa iliyokuwa Kliniki ya Tiba Asilia ya Fore Plan, Tabibu Juma Mwaka ‘Dk. Mwaka’, Jeshi la Polisi linadaiwa kumfungia kazi kwa msako mkali wa kumkamata.

Ijumaa iliyopita, Waziri Kigwangallah alifika kwenye kliniki hiyo iliyopo Ilala- Bungoni jijini Dar na kuliagiza Jeshi la Polisi kumsaka na kumkamata Dk Mwaka kisha kumfikisha mahakamani mara moja kwa kukiuka taratibu za kitabibu za tiba asilia licha ya kufungiwa lakini amekuwa akiendelea kutoa huduma hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum HamduniKamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Salum Hamduni.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilieleza kuwa askari wa jeshi hilo Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, wikiendi iliyopita waliendesha msako mkali wa kumkamata Dk. Mwaka huku wakiweka ulinzi kwenye kliniki hiyo ili endapo angefika wamkamate.

“Baadaye askari waligawanyika, wapo waliokwenda nyumbani kwake (Mbezi- Beach) lakini hawakumkuta hivyo wakaweka doria maeneo hayo ili akifika tu wamkamate.

“Mbali na huko, pia askari walipita kwenye viwanja vyake anavyopenda kujirusha wikiendi hasa kwenye klabu moja maarufu iliyopo Mikocheni (Dar) bila mafanikio.

“Pia waliweka ‘patroo’ kwenye uwanja wa ndege (JKIA) ili asipite kwenda nje ya nchi,” alisema mtoa habari wetu.

Akizungumza na Wikienda muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni juzi (Jumamosi) juu ya msako huo wa Dk. Mwaka, Kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdani alisema kuwa ni kweli polisi walikuwa wakimsaka jamaa huyo maeneo tofauti ikiwemo nyumbani kwake.

“Kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za mahali alipo Juma Mwaka atujulishe ili tumkamate mwenyewe,” alisema Kamishna huyo.

Tukio la kufungiwa kwa Dk. Mwaka siyo la kwanza kwani alishafungiwa mara mbili lakini baada ya muda aliendelea kutoa huduma kama kawaida hivyo kuibua mjadala mzito.

Profesor Jay “Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Magufuli Niliyoyaona ni Haya Hapa’

Leave A Reply