The House of Favourite Newspapers

Polisi Wanaume Wavalia Moka za Wanawake, Watinga Mtaani!

polisi-uganda-1

Maafisa kadhaa wa Jeshi la Polisi wa kiume nchini Uganda, jana Desemba 9, 2026 walivalia viatu vya kike na kushiriki katika matembezi kwa lengo la kuhamasisha jamii dhidi ya udhalilishaji na dhuluma dhidi ya wanawake.

Polisi hao walikuwa wanashiriki katika matembezi yafahamikayo kama ‘Walk A Mile in Her Shoes’ (Tembea Maili Moja na Kiatu Chake).

polisi-uganda-2Picha za maafisa waliovalia viatu hivyo zimesambazwa sana mtandaoni.

Polisi hao waliandaa matembezi hayo kwa ushirikiano na mashirika ya kutetea haki za wanawake.

polisi-uganda-3Shirika la Walk A Mile in Her Shoes linaloandaa matembezi hayo lilianzishwa mwaka 2001 na Frank Baird. Lilianza kama kundi la wanawake waliokuwa wakijitokeza na kutembea kwenye bustani wakiwa wamevalia viatu vya wanawake.

Lakini sasa limekuwa shirika kubwa na kila mwaka maelfu ya watu hushiriki kuchangisha pesa za kusaidia vituo vinavyowasaidia waathiriwa wa ubakaji, waathiriwa wa dhuluma nyumbani pamoja na miradi inayokabiliana au kupinga dhuluma na unyanyasaji wa wanawake.

halotel-strip-1-1

MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

Comments are closed.