The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakamata 11 Maandamano Ya Lissu Singida

0
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu.

Watu 11 wakiwemo madiwani wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya IKungi mkoani Singida wamekamatwa wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuishinikiza Serikali kutoa tamko kuhusu kuvamiwa na kupigwa risasi mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu amesema watu hao wamekamatwa na polisi leo Ijumaa mchana wakiwa na mabango katikati ya mji wa Ikungi, wakiwa kwenye harakati za kuhamasisha maandamano.

“Walitaka kufanya maandamano, tuliwawahi kabla hawajaanza, miongoni mwao wapo waliotokea Arusha na Dodoma, kwa hiyo wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi,” amesema Mtaturu.

Amesema tukio la Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi halijatokea Singida, hivyo hawataruhusu maandamano ya aina yoyote yanayoweza kuhatarisha amani.

Leave A Reply