The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakamata Watuhumiwa 586 Dar

1

Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akizungumza na wanahabari.

2

Sirro akiwaonyesha wanahabari baadhi ya vitu vilivyokamatwa.

3

Baadhi ya wanahabari wakichukua tukio hilo.

4

Baadhi ya vitu vilivyokamatwa katika matukio mbalimbali ya operesheni ya polisi.

DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya uharifu 586 waliokamatwa katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya msako mkali uliofanyika hivi karibuni jijini Dar kati ya Novemba 22 na Desemba 2, mwaka huu.

“Watuhumiwa waliokamatwa ni wa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi kutoka maungoni, kucheza kamari, kubughudhi abiria, wizi wa magari, kutengeneza, kuuza na kunywa pombe haramu ya gongo na mengineyo,” alisema Sirro na kuongeza:

“Pia kati ya Novemba 21 na Desemba 2, mwaka Jeshi la Polisi limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 878,670,000 kupitia tozo za makosa ya usalama barabarani.”

Na Denis Mtima/GPL

halotel-strip-1-1

Comments are closed.