The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakanusha Kuupiga Mabomu Msafara wa Lissu

0

JESHI la Polisi Mara, limekanusha uvumi kuwa msafara wa mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu umepigwa mabomu eneo la Nyamongo, mkoani humo leo Jumatatu, Septemba 28, 2020 wakati akielekea kwenye kampeni zake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, William Mkonda amesema mabomu yalipigwa kutawanya wafuasi waliokuwa wakiwashambulia askari wa jeshi hilo.

Taarifa zilizosambazwa na Chadema awali zilieneleza kuwa, Polisi wenye silaha wakiwa na magari zaidi 10 wamevamia na Kuushambulia msafara wa Mgombea Urais Mhe.Tundu Lissu leo Septemba 28, 2020 Nyamongo Serengeti mkoani Mara, wamepiga mabomu ya machozi na kujeruhi watu, Mhe. Lissu yupo salama taarifa zaidi zitawajia hapo baadaye.

Leave A Reply