The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakiri Kuwashikilia Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano ya Chadema

JESHI la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne limethibitisha kuwashikilia watuhumiwa watatu wenye majeraha ya risasi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 

Muliro amesema watuhumiwa hao ni wale waliokamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Februari 16 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini.

 

Aidha, kamanda huyo amekanusha taarifa ya kwamba majeruhi hayo hawajapatiwa matibabu tangu wakamatwe, amesema wote wamepelekwa katika hospitali za serikali hivyo hakuna asiyepatiwa matibabu kama inavyoelezwa.


Awali Mbunge wa Mikumi (CHADEMA), Joseph Haule aliandika kupitia Twitter na Facebook kuwa;

“Leo ni siku ya 9, Tangu Kamanda mwenzetu AIDA ULOMI apigwe risasi ya mguu, polisi bado wanamshikilia Kituo cha Oysterbay na wengine kadhaa bado wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali, Hajapelekwa mahakamani, hajapata matibabu yeyote na amegoma kula, twendeni tukamwone na kumsaidia…”

Aida Olomi aliyejeruhiwa.

Comments are closed.