POSH AFUNGUKA ALIVYUOMNASA MWANAUME WA ZARI

DAR ES SALAAM: Ama kweli mji mzito! Stori iliyotrendi vilivyo kwenye mitandao ya kijamii ni picha zilizomuonesha mrembo Jacqueline Obed ‘Poshy Queen’ akiwa na jamaa aliyesemekana ni mwanaume wa mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, King Bae. 

 

Katikakati ya mjadala mzito huku Poshy akiitwa nyakunyaku wa wanaume wa watu, gazeti hili lilimpata mrembo huyo na kufunguka anachokijua juu ya ‘saga’ hilo.

 

Picha hizo zilipoanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, watu wengi walipata mshtuko na kuanza kumtumia vijembe Zari kuwa anakwama wapi kutokana na kukwapuliwa wanaume wake huku ikiwa ni muda mchache tangu alipoanza kumnadi mwanaume huyo baada ya kuachana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Katika intavyu na gazeti hili, Poshy alifunguka alivyokutana na King Bae ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;

Risasi Mchanganyiko: Mambo vipi Poshy? Imekuwaje mpaka tena mambo ya kumuingilia Zari kwenye anga zake?

Poshy: Anga zipi tena? Nimemuingilia mimi?

Risasi Mchanganyiko: Kuna picha ambazo zinasambaa mitandaoni zikikuonesha ukiwa na King Bae wa Zari, hizo picha vipi?

Poshy: Jamaniii…kwani kupiga picha naye kuna tatizo?

Risasi Mchanganyiko: Hakuna tatizo, lakini ishu ni pozi tatra ulizoweka na huyo bwana, kwani ilikuwaje mkakutana?

Poshy: Yule tulianza kuchati, alikuwa na projekti fulani ndiyo akaja huku (Bongo) tukamalizana.

Risasi Mchanganyiko: Ni projekti gani hiyo?

Poshy: Huwezi kusema kitu cha mtu kabla hajaruhusu kukitaja maana labda anaona siyo wakati sahihi!

Risasi Mchanganyiko: Alipokuja Zari hapa Bongo alijua kuwa una projekti na King Bae?

Poshy: Sijui kwa kweli maana alikuja kikazi na sikuweza kumuuliza.

Risasi Mchanganyiko: Kwa hiyo bado mnawasilina?

Poshy: Ndiyo, lakini tunawasiliana kikazi zaidi.

Risasi Mchanganyiko: Asante sana Poshy.

Poshy: Poa, shukrani sana.


Loading...

Toa comment