POSHY QUEEN AFUNGUKA KUDAIWA NA BWANA WA ZARI

DAR ES SALAAM: Modo matata Bongo ambaye jina lake lilishika kasi ya umaarufu kutokana umbo lake la kiuno cha nyigu, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amemfungukia anayesemekana ni bwana mpya wa mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, King Bae.

 

Poshy ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa anashangazwa na madai kuwa jamaa huyo anamdai.

Poshy ameweka wazi kuwa, yeye na King Bae waliwekeana dau wakati Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Kenya zinacheza kwenye Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) hivyo walikubaliana kama Tanzania ingefungwa, Poshy angemlipa jamaa huyo kiasi fulani cha fedha, lakini hakufanya hivyo.

 

“Unajua ule ulikuwa ni utani tu, watu hata hawakuelewa ananidai nini, basi kila mmoja alishadadia, lakini ni mambo ya mpira na si kitu kingine kwa sababu tuliwekeana dau hivyo watu wasitokwe povu, wakajiuliza ninadaiwa nini mimi mpaka kwenye mitandao,” alisema Poshy ambaye hivi karibuni alidaiwa kumpora jamaa huyo kutoka kwa Zari.

 

Stori: IMELDA MTEMA, IJUMAA


Loading...

Toa comment