The House of Favourite Newspapers

Poulsen Awabadilishia Mbinu DR Congo

0

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema mchezo wa leo dhidi ya DR Congo, watabadili mbinu ili iwe rahisi kupata ushindi.

 

Leo Alhamisi, Taifa Stars itakuwa mwenyeji wa DR Congo katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo mashabiki 30,000 wameruhusiwa kuingia uwanjani.


Akizungumza na Spoti Xtra,
Poulsen alisema: “Mbinu ya kwanza ugenini tuliyoitumia haina maana tutaitumia tena,
kwa sasa siwezi kuiweka
wazi mbinu mpya, itajulikana uwanjani. Kikubwa ni kuona tunaweza kufanya vizuri na ipo wazi mchezo hautakuwa rahisi.


“Wachezaji wapo tayari
na malengo ni kuona tunashinda mchezo huu. Mashabiki wameruhusiwa kuja na tutakuwa nyumbani, hilo litaongeza nguvu kwa wachezaji kufanya vizuri.”

Kwa upande wa Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars, John Bocco, alisema wachezaji wamekubaliana kusaka ushindi,
hivyo mashabiki waendelee
kutuombea dua.


Kocha Mkuu wa DR
Congo, Header Cuper, naye alisema: “Tuna wachezaji wengi wazoefu ila haina maana kwamba tutawabeza wapinzani wetu, lazima tuje na mpango upo kwa kucheza bila kuogopa.”

WAANDISHI: HAWA ABOUBAKHARI, LUNYAMADZO MLYUKA NA CAREEN OSCAR

Leave A Reply