The House of Favourite Newspapers

PRETTY KIND AGEUKIA GOSPO

MSANII wa filamu na muziki wa Kizazi Kipya, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amegeukia kuimba muziki wa Injili ‘Gospo’ kwa kile alichosema amechoshwa na mambo ya duniani.

 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Pretty Kind alisema baada ya kumrudia Mungu, ameamua kuachana na muziki wa kidunia na sasa anaandaa nyimbo za Injili ambazo ataziachia hivi karibuni.

 

“Tangu nimeokoka maisha yangu yamekuwa ya furaha mno na nina amani moyoni tofauti na nilivyokuwa naendekeza maisha ya kidunia hivyo ili kudhihirisha furaha aliyonipa Mungu, sasa ninaanza kuimba nyimbo za Injili ili ziwe ushuhuda wa kuwabadili na wengine,” alisema Pretty Kind.

Mwandishi Wetu

Comments are closed.