The House of Favourite Newspapers

Pretty Sasa Ageukia Kuhubiri Injili

0

MSANII wa Bongo Fleva na filamu ambaye kwa sasa ameokoka; Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amefunguka kuwa, mwaka huu mpya wa 2020 ni wake wa kuhubiri Injili kwa njia ya uimbaji.

Akipiga stori na Gazeti la IJUMAA, Pretty alisema kuwa, kwanza anamshukuru Mungu kwa neema ya kuuona mwaka huu maana ni kwa neema tu, lakini pia anafurahi kuanza mwaka na Mungu ambapo anajipanga kwa ajili ya kuanza kutoa nyimbo za Injili.

“Huu ni mwaka wangu wa kuhubiri Injili kwa njia ya uimbaji, hivyo ninamuomba Mungu aniwezeshe maana nimeanza rasmi kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo za Injili,” alisema Pretty.

Leave A Reply