Prince Dube Ataja Kinachomtesa VPL

STRAIKA wa Azam FC, Prince Dube amefunguka kuwa hafurahii timu yake inapocheza kwenye baadhi ya viwanja vya mikoani kutokana na kwamba haviifanyi timu hiyo kucheza mpira ambao ameuzoea.

 

Straika huyo ameongeza kwamba katika viwanja hivyo pia wachezaji wanaovitumia wamekuwa wakitumia nguvu zaidi tofauti na wakikutana kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex.

Dube mwenye mabao matano katika Ligi Kuu Bara hadi sasa kabla ya matokeo ya michezo ya jana, ameitumikia Azam FC michezo mwili mikoani dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine na dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

 

Straika huyo raia wa Zimbabwe amesema: “Mechi za Chamazi (Azam Complex) nazifurahia kwa sababu nimeshauzoea uwanja na ni rafiki kwa mchezaji yeyote.

 

“Lakini mkoani viwanja vyake ni vigumu kwa sababu haviko na usawa mzuri, vinasababisha timu kucheza mipira ya juu hivyo ni vigumu kufurahia mchezo mzuri wa pasi za chini, pia kuna matumizi makubwa sana ya nguvu,” aliweka nukta Dube.

Toa comment