The House of Favourite Newspapers

Prof Jay Afungukia Shoo Yake ya Kwanza Tangu Awe Mbunge – Video

 

MBUNGE wa Mikumi (Chadema) na rapa maarufu Afrika Mashariki na Kati, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amefunguka na kusema kuwa ataandika Historia mpya na ya ki[pkee kwenye game ya muziki wakati wa shoo yake ya kwanza tangu awe Mbunge.

 

Profesa Jay ambaye anatarajiwa kufanya shoo yake hiyo hivi karibuni jijini Mwanza, amesema alimisi jukwaa, aliwamisi mashabiki zake, hivyo watu wote wa Kanda ya Ziwa wategemee mambo makubwa na sapraizi ya aina yake kwenye shoo hiyo.

 

Katika Shoo hiyo iliyoandaliwa na Sports Music and Festival, inatarajiwa kufanyika siku ya Iddi Mosi huku mashabiki zake wakiwa na hamu ya kumuona aki-perform jukwaani kwani ni kitambo amekuwa kimya kutokana na majukumu ya ubunge anayowawakilisha wananchi wake.

 

MSIKIE PROF. JAY AKIFUNGUKA

Comments are closed.