The House of Favourite Newspapers

Breaking: Lipumba Apitishwa Kugombea Uenyekiti CUF

 

BARAZA Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) leo limewapitisha wanachama watatu wa chama hicho akiwamo Profesa Ibrahim Lipumba kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.

 

Wagombea wengine  nafasi ya uenyekiti ni Diana Daudi Simba na Zuberi Mwinyi Hamisi. Mkutano huo ambao ulifanyika katika ukumbi wa Lakem, Buguruni, jijini Dar es Salaam,  umehudhuriwa na wajumbe 798.

 

Naye Mkurugenzi wa habari wa CUF, Abdul Kambaya,  amesema kinachoendelea  ni kuchagua wajumbe watakaoshiriki uchaguzi huo.

 

Kambaya amesema hali ya leo katika mkutano huo ilikuwa nzuri tofauti na ilivyokuwa jana. Pia amesema kutakuwepo na ulinzi wa askari ambao watakuwa wamevaa nguo za kiraia ili kuhakikisha hali ya usalama inakuwapo.

 

CUF upande wa Lipumba, wanafanya uchaguzi huku kukiwa na mgogoro ambapo upande unaomsapoti Katibu Mkuu wa chama hicho wakipingana na mkutano huo kwa madai kwamba Lipumba hana uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama hicho tangu alipotangaza kujivua nafasi hiyo.

 

Vilevile, mchakato huo umefanyika wakati chama hicho kikisubiri uamuzi wa Mahakama Kuu ambao unategemewa kumaliza mvutano wa muda mrefu baina ya pande hizo.  Uamuzi huo ulioahirishwa kutolewa mwezi uliopita (Februari), unategemwa kutolewa mwezi huu.

Comments are closed.