The House of Favourite Newspapers

Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon watangaza Mshindi ..

Afisa Mauzo wa Kampuni ya Kansai Plascon (T) Ltd, FloraMapunda,akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi, Robson Majura, mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon

Dar es Salaam: Promosheni ya Paka Rangi ya Plascon na Ushinde imerejea, na sasa inakuja na toleo maalumu la rangi, maarufu kama Rangi ya Pesa kwa nia njema ili kuwanifaisha wateja wake. Mwaka huu washindi watajishindia na zawadi za pesa taslimu.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Hussein Jamal, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo kipya cha mauzo ya rangi ya Plascon, jijini Dar es Salaam. Jamal alisema, “Kibiashara tunafurahi kuwa na kampeni kama hii ambapo kupitia katika promosheni yetu , tuna uhakika kwamba, kuwapo na ushindi wa pesa taslimu kutaleta nyuso za furaha kwa washindi katika kipindi chote cha msimu wa kampeni hii.

Muwakilishi kutoka kampuni ya Plascon Mkoani Mwanza Subodh Issar akimkabidhi Frank Silver mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon

Promosheni ya Paka Rangi na Ushinde inatupatia fursa, siyo tu kuwazadia wateja wetu muhimu, watumiaji wa rangi na wauzaji, lakini pia kujenga msingi wa mafanikio ambayo tumeyapata kupitia bidhaa yetu ya hii ya Plascon, tangu tulipoizindua mwaka 2017,”

Kadhalika, Jamal alifafanua kuwa, promosheni hiyo ni ushahidi tosha wa kuonesha jinsi ambavyo Plascon imeamua kutoa huduma kwa watanzania na namna biashara yake inavyolenga kuongeza thamani katika uzalishaji wa rangi bora, zenye viwango, utafiti na wenye lengo la kukidhi haja ya mahitaji ya rangi na kutoa ushauri bora kwa watanzania na watumiaji wa rangi kwa ujumla.

Promosheni iliyopewa jina la ‘Colour of Money’ itaendeshwa kuanzia Otoba 7 hadi Desemba 14, 2019, na inatarajia kushirikisha mamia na maelfu huku kila mshiriki akiwa na uhakika wa kutotoka mikono mitupu . Meneja Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Tyron Immelmann, alisema kuwa, mwaka huu , Plascon itatoa zawadi za pesa taslimu shilingi milioni tano kila wiki, ambapo kila siku kutakuwa na mshindi wa Sh 1,000,000 taslimu.

Washiriki watatakiwa kununua lita 20 za rangi ya Plascon, na kupewa kadi ambayo mteja ataisugua na na kutuma namba zake za bahati kwenda 15054, baada ya hapo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi. Matangazo ya Msimu huu wa Promosheni ya Paka Rangi Ushinde na Rangi ya Pesa, yatatangazwa kupitia vipeperushi kutoka kwa wauzaji, halikadhalika kupitia katika radio na televisheni.

Comments are closed.