The House of Favourite Newspapers

PSG: Kikosi Ghali Zaidi Ligue 1

0

 

MTANDAO wa Transfermarkt, umetoa orodha ya kikosi ghali zaidi ndani ya Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’. Katika kikosi hicho, kuna wachezaji nane wa PSG.

 

Mchezaji ghali zaidi ndani ya kikosi hicho ni Kyllian Mbappe ambaye thamani yake ni euro milioni 200, huku Neymar akifikia euro milioni 160 akiwa ndiye mchezaji wa pili kwa thamani kubwa.

Kikosi kamili cha wachezaji ghali zaidi ndani ya Ligue 1 kwa msimu huu hiki hapa:

 

  1. ANTHONY LOPES

Mlinda mlango ni Anthony Lopes wa Lyon. Thamani yake kwa sasa ni euro milioni 22, thamani yake imeshuka kutoka euro milioni 25.

 

  1. THOMAS MEUNIER

Beki wa kulia ni Thomas Meunier wa PSG ambaye thamani yake ya euro milioni 30.

 

  1. JUAN BERNAT VELASCO

Beki wa kushoto ni Juan Bernat Velasco kutoka katika timu ya PSG. Thamani yake ni euro milioni 20 ikiwa imepanda kutoka euro milioni 15.

 

  1. ABDOU DIALLO

Abdou Diallo ni beki wa kati kutoka PSG, thamani yake ni euro milioni 35.

 

  1. MARQUINHOS

Euro milioni 65 ndiyo thamani yake. Katika kikosi hiki, anakuwa sambamba na Abdou Diallo katika beki wa kati. Naye ni mchezaji wa PSG.

 

  1. MARCO VERRATTI

Kiungo cha kati anasimama Marco Verratti wa PSG ambaye thamani yake ni euro milioni 75.

 

  1. KYLIAN MBAPPE

Winga ya kulia anacheza Kylian Mbappe wa PSG ambaye thamani yake ni euro milioni 200.

 

  1. HOUSSEM AOUAR

Houssem Aouar wa Lyon ambaye thamani yake ni euro milioni 50 akipanda thamani kutoka euro milioni 45, anacheza kiungo cha kati sambamba na Marco Verratti.

 

  1. MAURO ICARDI

Mshambuliaji wa kati ni Mauro Icardi wa PSG ambaye thamani yake ni euro milioni 75.

 

  1. MEMPHIS DEPAY

Memphis Depay atacheza sambamba na Icardi. Depay wa Lyon, thamani yake ni euro milioni 55 akipanda thamani kutoka euro milioni 45.

 

  1. NEYMAR

Winga ya kushoto anachukua Neymar ambaye ni wa pili kwa thamani kubwa. Thamani yake ni euro milioni 160 akishuka kutoka euro milioni 180.

PARIS, Ufaransa

 

Leave A Reply